Akizungumza na mwandishi wa habari hii katika mahojiano maalum, Ray
alisema: “Kama nitakuwa sijajifunza kitu kutokana na msiba wa Kanumba
(Steven) nitakuwa mjinga. Kama utakumbuka, kwenye mazishi yake serikali
nzima ilikuwa pale, umati mkubwa wa watu ulifurika, kwa nini? Kwa
sababu ya thamani yake.
“Msambazaji aliye ‘serious’ ni mmoja kwa
sasa na yeye ndiye anayeamua cha kufanya na kwa sababu wasanii tupo
wengi, hatuna jinsi. Ukiingia naye mkataba unakuwa umeuza haki ya maisha
yako yote. Anakuwa na uhuru wa kupeleka DSTV, Zuku na Channel nyingine
zozote bila kukulipa chochote.
“Lakini mimi siwezi kutupa lawama
kwa serikali maana tumeshaongea sana. Nawaomba wadau wajitokeze wawekeze
kwenye tasnia yetu maana inapanuka na ina soko kubwa ila msambazaji
yupo mmoja tu ndiyo maana tunanyonywa.”
No comments:
Post a Comment