Thursday, June 13, 2013

"WANAFIKI WANAENEZA HABARI KWAMBA LWAKATARE ATAFANYA MKUTANO WA HADHARA. HUO NI UONGO".... CHADEMA



Kumekuwepo na taarifa zinazosambazwa kwa njia mbalimbali za upashanaji habari tangu jana juu ya vitu viwili ambavyo vyote vinamhusu Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Ndugu Wilfred Mganyizi Lwakatare.
1. Kwamba atafanya press conference leo, (watu wale wa upande wa pili wameenda mbali hata wametaja muda eti ni saa 4 asubuhi)


2. Atakuwa kwenye mizunguko ya mikutano ya kampeni katika chaguzi ndogo za udiwani zinazoendelea katika hatua ya lala salama maeneo mbalimbali nchini.


Usahihi.


Kwa kuzingatia masuala kadhaa hasa mikakati ya kitaalam katika mapambano ya kisiasa, hususan katika suala hili, press conferense iliahirishwa tangu jana mapema asubuhi, baada tu ya baadhi ya vyombo vya habari kuwa vimetangaza kuwa itafanyika leo, Alhamis. Tuliviarifu vyombo vya habari hivyo. Imesogezwa mbele na taarifa zitatolewa tena.


Suala la mizunguko kwenye kampeni za uchaguzi mdogo...hakuna kitu kama hicho kwa sasa.


Pamoja na kwamba kuna watu wenye mapenzi mema kabisa na vuguvugu la mabadiliko wamekuwa na hamu ya kutaka kumsikia kamanda mwenzao, ndugu Lwakatare akizungumza majukwaani baada ya miezi mitatu ya 'ukatili' mkubwa, pia tumebaini kuwa watu wa upande wa pili, wanataka sana kujua CHADEMA sasa inajua kiasi gani juu ya njama za kuibambikia ugaidi, utekaji na mauaji.


Hivyo upande huo wa pili, ambao unaonekana dhahiri kuwa under pressure ya kutojua kiasi gani mipango yao inajulikana na itaumbuliwa kwa kiwango kipi, umekuwa ukieneza habari za Lwakatare kufanya mikutano ya hadhara kwenye kampeni za uchaguzi wa madiwani, kitu ambacho si kweli.


Baada ya hila na uovu wa watawala na vibaraka wao kushindwa katika jaribio lingine kubwa kabisa wao kuwahi kupanga dhidi ya wimbi la mabadiliko na kutaka kuzuia kasi ya CHADEMA kuwaondoa madarakani, tumwache ndugu Lwakatare apumzike na familia, wakati mipango makini ikifanywa kwa ajili ya matukio yote mawili ambayo Watanzania wanategemea na kuyasubiri kwa hamu yafanyike; mkutano na press conference.


Kitu kimoja cha uhakika ni kwamba, watu wa upande wa pili, ambao tayari hofu yao inajulikana, hawataweza kumchagulia Lwakatare wala kuichagulia CHADEMA kitu gani cha kusema, kama ambavyo wameanza kufanya kupitia forums mbalimbali. Let them cool down, wasiwasi wa nini! Yote yakayosemwa itakuwa ni kwa ajili ya maslahi ya Watanzania, haitakuwa kwa ajili ya kuifurahisha 'status quo'.


Ukweli haujawahi kushindwa na uongo, wala dhuluma haijawahi kuishinda haki. Vyote viwili, ukweli na haki, vinaweza kuchelewa tu, lakini hatimaye huwadia. Kwa sababu Lila na Fila havitangamani.


Makene
  via jamiiforum
0752 691569


No comments:

Post a Comment