Wednesday, June 12, 2013

LWAKATARE AMEACHIWA KWA DHAMANA YA MILIONI 10



Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Muganyizi Lwakatare ameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 10 leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar. 
Lwakatare anakabiliwa na kesi ya kujaribu kumwekea sumu Dennis Msaki. Waliomuwekea dhamana Lwakatare ni madiwani wawili wa Chadema kutoka kata ya Kimara na Sinza. 
Madiwani hao wametakiwa kuhudhuria mahakamani kila kesi hiyo itakapotajwa.

No comments:

Post a Comment