Mambo yamwendea mlama msanii kutoka Tanzania Mr.Nice ambae
alikuwa ameula katika nchi jirani ya
Kenya kwa kusaini mkataba mnomo na familia kubwa ya Muziki ya GrandPa Records
inayowapeleka mbele sana wasanii kadhaa akiwemo DNA, Ng’ang’a wa TPF na
wengine.
Mr. Nice amepigwa chini na Familia hiyo ambayo tayari
ilikuwa imeshampigisha hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kumuandalia tour ya
kumtambulisha nchi nzima kwa lengo la kumuongezea mashabiki, kumpa show ya
kumtambulisha na kuachia ngoma moja aliyofanya na DNA “Tafuta”.
Grandpa Records kupitia C.E.O wao bwana Refigah wametoa
tamko rasmi ambalo limetaja sababu za kumtema ikiwa ni pamoja na kuwa ni msanii
huyo alikuwa ameshasaini mkataba na studio za Fishcrab chini ya Lamar na Sallam
Sharaf na wakati anasaini mkataba na Grandpa
Records hakuweka wazi.
Kupitia tamko hilo Grandpa Records wamemuelezea Mr.Nice kama
msanii mvivu, asiye na ushirikiano, asiyetegemewa na mgumu kuliko wasanii wote
waliowahi kufanya kazi chini ya Familia hiyo.
Kwa mujibu wa mtandao wa ghafla, baada ya tamko hilo kufikia
vyombo vya habari, C.E.O wa Grandpa Records aliitwa studio za Citizen radio na
kufanya mahojiano na mtangazaji maarufu Willy M. Tuva kuelezea kwa undani
sakata hilo, na mtangazaji huyo alipompigia simu Mr.Nice ili kupata maelezo kwa
upande wake pia aligeuka mbogo na kutoa maneno kwa hasira akitishia kumbomoa
mtu, na kwamba yeye sio wale wa ‘nyenyenyenyee’, msitari wa wimbo wa GrandPa
family ‘Fimbo ya Pili’.
Hili ndilo tamko lililotolewa na GrandPa Records:
“To Grandpa Records fans and friends we've decided to drop
Mr nice from Grandpa Records artists' roster. Mr Nice has been terminated for
violating the agreement we entered with him.
For the sake of media and the
general public we will summarize and say this, Mr Nice is the most difficult,
uncooperative, lazy, unreliable artist we've ever worked with. The points and
incidents of conflict are too many to mention here.
To be brief Mr Nice had
previously signed a deal with Sallam Sharaf and Lamar in Tanzania and did not
disclose this to us at the point of being signed to grandpa records. All in
all, aluta continua we tried our best but he failed us.”
No comments:
Post a Comment