Monday, May 6, 2013

LADY JAYDEE AWAFANYA CLOUDS FM WAGOME KUPIGA NYIMBO YOYOTE YA BONGO FLEVA.....TIMES FM WASHANGILIA



 Akizungumza  katika kipindi cha Power Breakfast, Meneja wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ameelezea kuwa Lady Jaydee  amekosea  kuelekeza  vita  kwao...


Amedai  kuwa kama tatizo ni Bendi ya SkyLight basi apambane kuipiku bendi hiyo na si kugombana na watu wengine.....

Akiongea  kwa  mbwembwe, Ruge  ameamuru  kutopugwa  wimbo  wowote  wa  bongo  fleva  leo.....

Amesema kuwa Clouds  fm ni chombo binafsi kina maamuzi ya kufanya chochote pasipo kuvunja sheria...
Baada  ya  kauli  hiyo  Times Fm  wamewajibu  clouds  fm  na  kudai  kuwa  WAO  LEO  WATAPIGA  BONGO  FLEVA  MPAKA  MAJOGOOOO...!!!   
Nadhani  Times  fm  wamefikia  uamuzi  huo  ili  kuwajulisha  clouds  kuwa  kuna  vituo  vingine  vingi vya  radio  zaidi  yao  na  kwamba  hawako  peke  yao 
Hii  ndo  tweet  yao...

 
"Kwa Kutumia Kilicho chetu , Asili yetu na Muziki wetu leo katika vipindi vyote utaskikia muziki wa nyumbani wa BONGO FLEVA kwa asilimia Kubwa."

No comments:

Post a Comment