Mbunge
wa Arusha Mjini Godbless Lema ameachiwa kwa dhamana hivi punde baada ya
kushtakiwa kwa makosa ya uchochezi katika mahakama ya Mkoa wa Arusha huku
maandamano yakifanyika hivi sasa katika mitaa ya Jiji la Arusha, Tanzania.
Katika Mahakama hiyo kulikuwa na umati mkubwa wa wafuasi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Mashabiki, wafuasi na wanachama wa chama hicho walifurika katika mahakama hiyo kwa ajili ya kumuunga mkono mbunge huo.habarimasai.com itaendelea kukuletea Taarifa zaidi baadaye.

Hivi
sasa mashabiki, wafurukutwa na wanachama wa Chadema wanafanya maandamano
makubwa kuelekea katika ofisi za chama hicho ambazo zipo katika eneo la
Ngarenaro.
Hivi
sasa wanapita katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mulongo kwa maandamano
huku wakipiga kelele za kuzomea.
Kesi
ya uchochezi dhidi ya Lema imefunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mkoa
wa Arusha na endeshwa na Hakimu Devota Msoffe.
Mwandishi
wetu anasema kwamba kesi hiyo imeahirishwa mpaka Mei 29 mwaka huu.
Katika hati ya
mashtaka ambayo ipo katika mahakama hiyo inasema kwamba kosa la Lema ni ' kutoa
maneno yanayodaiwa kuwa ni uchochezi.
No comments:
Post a Comment