Monday, April 29, 2013

"LAZIMA TUZIKAGUE KUCHA ZA LEMA..... TUPO TAYARI KUFA....."HAYA NI BAADHI YA MABANGO YA WAANDAMANAJI HUKO ARUSHA


KITENDO CHA WANAWAKE KUNYONYANA NDIMI HUKU WAKIWA NUSU UCHI KIMEMFANYA PREZZO AIPITIE UPYA VIDEO YAKE


MWANAUME AZIKWA AKIWA HAI JIJINI MBEYA KWA MADAI KUWA NI MCHAWI


KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa kijiji na kata ya Mkwajuni Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya  wamemzika Mwanakijiji mwenzao akiwa hai wakimtuhumu kusababisha kifo cha Mkazi mmoja kijijini hapo. 
 
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Apri 26 mwaka huu majira ya Saa Nane Mchana katika Kitongoji cha Maweni Makaburini baada ya Mhanga aliyefahamika kwa jina la Victory Mwachirui(68) kuhudhuria mazishi ya Pita Barton(28)aliyefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.

 
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Thobias Ismail amesema marehemu alipatwa na mauti akiwa anapatiwa matibabu kwa mganga wa jadi ambaye jina lake halikuweza kujulikana maramoja.


Amesema wakati taratibu za mazishi zikiendelea Ndugu wa marehemu walidai kuwa kifo cha Marehemu kilisababishwa na Mwachirui ambaye ni Katekista mstaafu kwa imani za kishirikina.


Ameongeza kuwa wakati kaburi likichimbwa kwa ajili ya kumzika marehemu ndipo vijana waliokuwa wakichimba waliagiza Wazee wa Mila wafike makaburini kwa ajili ya kuangalia utaratibu wa mazishi na kukagua ukubwa wa Kaburi ambalo lilikuwa limekwisha chimbwa.



Kutokana na mwito huo walifika wazee wanne akiwemo Mzee Mwachirui ambaye walimsisitiza kusogea jirani na kaburi ambapo baada ya kusogea alipigwa na Sururu kichwani na kuangukia kaburini huku akisindikizwa na marungu..

Jeneza la aliyekufa kwa ugonjwa tayari limetolewa pembeni. Sasa anafukuliwa aliyezikwa akiwa hai
Jeneza la aliyekufa kwa ugonjwa tayari limetolewa pembeni. Sasa anafukuliwa aliyezikwa akiwa hai

                     Mwili wa aliyezikwa hai unatolewa kaburini 
Mwili wa aliyezikwa hai unatolewa kaburini

                     Dada wa marehemu aliyezikwa akiwa hai
Dada wa marehemu aliyezikwa akiwa hai

MAANDAMANO MAKUBWA YANAENDELEA JIJINI ARUSHA BAADA YA GODBLESS LEMA KUACHIWA HURU





Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ameachiwa kwa dhamana hivi punde baada ya kushtakiwa kwa makosa ya uchochezi katika mahakama ya Mkoa wa Arusha huku maandamano yakifanyika hivi sasa katika mitaa ya Jiji la Arusha, Tanzania.

Katika Mahakama hiyo kulikuwa na umati mkubwa wa wafuasi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Mashabiki, wafuasi na wanachama wa chama hicho walifurika katika mahakama hiyo kwa ajili ya kumuunga mkono mbunge huo.habarimasai.com itaendelea kukuletea Taarifa zaidi baadaye.
 
Hivi sasa mashabiki, wafurukutwa na wanachama wa Chadema wanafanya maandamano makubwa kuelekea katika ofisi za chama hicho ambazo zipo katika eneo la Ngarenaro.

Hivi sasa wanapita katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mulongo kwa maandamano huku wakipiga kelele za kuzomea.

Kesi ya uchochezi dhidi ya Lema imefunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mkoa wa Arusha na endeshwa na Hakimu Devota Msoffe.

Mwandishi wetu anasema kwamba kesi hiyo imeahirishwa mpaka Mei 29 mwaka huu. 

Katika hati ya mashtaka ambayo ipo katika mahakama hiyo inasema kwamba kosa la Lema ni ' kutoa maneno yanayodaiwa kuwa ni uchochezi. 

PADRI WA KANISA KATOLIKI HUKO MOSHI AFUMANIWA LIVE NA MKE WA MTU AKIWA UCHI WA MNYAMA


KANISA Katoliki Jimbo la Moshi limeingia katika kashfa nzito baada ya padri wake, Father Urbanus Ngowi wa moja ya parokia zake kudaiwa kufumaniwa na mwanamke anayesemekana ni mke wa mtu

Father Ngowi akiwa ameduwaa baada ya kufumaniwa akiwa na mke wa mtu aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.
Sakata la fumanizi hilo linadaiwa kutokea Jumatatu ya wiki iliyopita chumbani kwa padri huyo, Marangu Wilaya ya Moshi  Vijijini ambako Father Ngowi inasemekana alikutwa ‘laivu’ akiwa na mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.

Pamoja na kunaswa huko, vyanzo havijaeleza humo chumbani wawili hao walikuwa wakifanya nini!


Habari zinadai siku ya tukio, mwanamke huyo aliingia nyumbani kwa padri huyo ambapo baadhi ya ndugu wa mumewe walikuwa wakimfuatilia baada ya madai yaliyokuwepo kwamba ana ukaribu wenye maswali mengi na mtumishi huyo wa Mungu.


“Unajua siku nyingi ilivuma kwamba Mama P na Father Ngowi wana ukaribu wenye maswali mengi, mume wake alifuatilia na kubaini ni kweli lakini akashindwa kuutenganisha ukaribu wao,” kilidai chanzo.

Father Ngowi akijaribu kuomba samahani baada ya kufumaniwa.
Chanzo kikaendelea kudai kwamba baada ya kuona mkewe amejikita kwa mtumishi wa Mungu, mumewe alinyoosha mikono juu na kumwachia Mungu.

Chanzo: Sasa siku hiyo baada ya ndugu wa mume kumfuatilia mpaka anaingia kwa Father Ngowi, wakaona ni bora watafute mpigapicha ili kupata picha za tukio ambazo zitakuwa ushahidi siku za mbele.


“Walipompata wakazama ndani, sekeseke likaanzia hapo. Walimkuta mwanamke huyo na mtumishi wa Mungu wapo kitandani.”

 
Father Ngowi na Mama P wakivaa nguo zao kwa aibu baada ya kufumaniwa.

Habari zinadai kwamba kufuatia tukio hilo, tayari Kanisa Katoliki limemweka kitimoto padri huyo ambaye alikuwa akihudumu katika Parokia ya Korongoni, Moshi Vijijini kabla ya kuhamishwa na kupelekwa Parokia ya Makomu, Marangu ambako inadaiwa ameshushwa cheo.


Inadaiwa kuwa baada ya tukio hilo, Father Ngowi alikana kukutwa na mke wa mtu chumbani kwake lakini alipobanwa sana na mabosi wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Moshi, alikiri na kudai ibilisi alimpitia na kuomba kanisa limsamehe na kutompa adhabu kali ambayo itamuathiri kisaikolojia.


Hili ni tukio kubwa na la aina yake kuwahi kulikumba Kanisa Katoliki nchini kwa padri wake kudaiwa kukutwa na mke wa mtu chumbani kwake!

Father Ngowi na Mama P wakiwa na nyuso za aibu baada ya tukio hilo.

Kuna madai kwamba mwaka jana (2012), Father Ngowi, mbele ya waumini wake alisoma barua yenye kukana shutuma zote zilizoelekezwa kwake kwamba amekuwa na ukaribu wenye maswali mengi na wake za watu.


Taarifa zilidai kuwa padri huyo aliweka wazi akisema si kweli kwamba amekuwa na ukaribu unaotajwa, akawataka waumini wake wapuuze tuhuma hizo alizosema  zina mwelekeo wa kuchafua sifa yake na taswira ya Kanisa Katoliki kwa jumla.


Hayo ni madai ya vyanzo vyetu ambavyo viliambatanisha na picha mbalimbali za tukio hilo lenye kushtua waumini sambamba na namba za simu za padri huyo kwa ajili ya mawasiliano ili kujiridhisha.

                                     Father Ngowi akipatiwa suruali yake.

MBUNGE LEMA AZUILIWA KUPIGA MSWAKI WALA KUNYWA CHAI......





TUKIO la kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), kwa madai ya uchochezi, limeibua sura mpya baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutajwa kuwa nyuma ya mkakati huo,
 
Lema ambaye bado anaendelea kusota rumande siku ya tatu baada ya kunyimwa dhamana, ameanza kufanyiwa vituko na Jeshi la Polisi baada ya jana asubuhi mkewe kuzuiliwa asimpe mswaki wala chai.
 
Mbunge huyo alikamatwa kutokana na amri ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, aliyedai kuwa aliwachochea wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha kumzomea kiongozi huyo na kupopoa gari lake kwa mawe.
 
Hata hivyo, siku moja kabla ya kukamatwa Lema aliwaonesha waandishi wa habari ujumbe mfupi wa simu ya kiganjani aliyotumiwa na Mulongo akimtishia kuwa atamfungulia kesi yoyote anayoitaka.
 
“Umeruka kihunzi cha kwanza, nitakuonesha kuwa mimi ni serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi,’’ ulisomeka ujumbe huo uliotumwa kupitia simu namba 0752 960276 ambayo Lema alidai ni ya Mulungo.
 
Pia nguvu kubwa iliyotumika kumkamata mbunge huyo usiku saa 5:30 kwa kutumia askari na maofisa wa usalama kuzingira nyumba yake, imehojiwa na baadhi ya wananchi, wakitilia shaka kuwa kuna siri ndani yake.
 
Madai ya Mulongo kuwa Lema alichochea wanafunzi hao yanakinzana na ushahidi wa video unaoonesha kuwa mbunge huyo alitumia kila aina ya ushawishi kuwasihi wasiandamane baada ya mwenzao, Elly Kago (22), kuuawa na watu wasiojulikana jirani na chuo hicho.
 
Akizungumza na gazeti hili jana, mke wa Lema, Neema, alisema kuwa alifika kituo cha polisi asubuhi akipeleka chai, lakini akaelezwa kuwa haruhusiwi kumpelekea chai.
 
Alisema kuwa alipiga simu kwa mkuu wa upelelezi wa mkoa ndipo akaambiwa ampelekee na alipofika tena kituoni askari aliyekuwa zamu alianza kupekua mfuko wa Neema kwa fimbo, kisha akaamuru Lema apewe, ila anywe kwa dakika tatu.
 
Wakati anafungua chupa ya chai na kumimina kwenye kikombe, askari alimweleza kuwa imebaki dakika moja, hatua iliyomuudhi Lema akidai ni udhalilishaji, hivyo akashindwa kunywa.
 
Alipotaka kupewa mswaki, askari alikataa kuwa vifaa hivyo vinaweza kutumika kama silaha, hivyo haruhusiwi kupewa.
 
Tanzania Daima Jumapili lilizungumza na wanasheria kadhaa pamoja na wanasiasa wabobezi kuhusu sakata hilo, ambapo baadhi walidai huo ni mkakati wa CCM kutaka kuidhoofisha CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa madiwani ujao kwenye kata nne.
 
“Kesho mnaweza kusikia Lema akifunguliwa kesi ya ajabu ya kutunga halafu kwa kipindi hiki kampeni zikianza mahakama itakuwa ikiisikiliza mfululizo ili asipate nafasi ya kushiriki kikamilifu.
 
“Huu mkakati si wa Mulongo peke yake bali ni mbinu za CCM zilizobakia katika kuhakikisha wanaikamata Arusha. Lakini naona kama wanazidi kujimaliza,” alisema mwanasiasa mmoja aliyeomba kuhifadhiwa jina lake.
 
Mwanasiasa huyo kutoka mkoani Arusha aligusia pia mkanganyiko wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) hivi karibuni kutangaza kata nne kurudia uchaguzi na kuiacha moja ya Sombetini ambayo diwani wa CCM alihamia CHADEMA.
 
“Ujue CCM wanafanya mambo bila kupima athari, Arusha ni mji wa kitalii lakini kwa sasa unaogopeka kwa fujo za polisi na wanasiasa, hata kesho utaona wakati Lema akipelekwa mahakamani.
 
“Hapa ni ngome ya CHADEMA hata kama Lema hayupo, sasa NEC wameibana Sombetini kwa hofu kuwa kata zote zikienda CHADEMA watakuwa na madiwani zaidi ya CCM, hivyo ishu ya meya kufufuka upya, ndiyo wakaamua kumtumia Mulongo kufanya mchezo huu wa hatari,” alisema.
 
Alipopigiwa simu jana jioni na kuulizwa juu ya madai hayo, Mulongo alizungumza kwa ukali akisema: “Wewe mhariri unaweza kunipigia simu kuniuliza swali kama hilo?”..
 
Aliendelea kufoka akisema: “Acheni kufanya kila kitu siasa, wewe ni polisi kujua Lema kwanini akamatwe hivyo, niache mimi niko na wageni wangu,” alisema na kukata simu.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Francis Stolla, alizungumzia suala la kukamatwa kwa Lema akisema kuwa nguvu kubwa na utaratibu uliotumika kumkamata haukuwa wa busara.
 
Stolla alisema: “Kwa mujibu wa kifungu cha 58 na 59 vya sheria ya ushahidi, Jeshi la Polisi au hata kama ni kwa amri ya mkuu wa mkoa ya kukamata walipaswa kuchagua njia nyingine ya busara.
 
“Jeshi linaweza kuwa na mamlaka mapana ya kukamata au hata kama ni kwa amri ya mahakama, busara huhitajika kutumika. Lema ni mbunge, anafahamika na upatikanaji wake hauna utata, anapotuhumiwa kuhitajika polisi busara inatumika kumwita au kumwandikia aende, si kumvizia kama walivyofanya,” alisema.
 
Mwanasheria mwingine ambaye aliomba kuhifadhiwa jina, alifafanua kuwa: “Rais peke yake ndiye Amiri Jeshi. Uamiri jeshi wa rais haugawanyiki mpaka kwa wakuu wa mikoa.
 
“Uamiri jeshi wa rais upo kikatiba, hauwezi kuwa wa wakuu wa mikoa au wa wilaya. Ndiyo maana anayeamrisha polisi katika mkoa ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa, na wilayani anakuwapo ofisa anayeamrisha (OCD),” alisema.
 
Aliongeza kuwa sheria zinaruhusu mkuu wa mkoa na wilaya kutoa amri ya kukamata mtu kama hakuna askari lakini mtuhumiwa anapokamatwa sharti aambiwe anakamatwa kwa kosa lipi na anayemkamata ajitambulishe.
 
Alisema kuwa siku ya tukio chuoni, polisi walikuwapo wakati Lema akizungumza na wanafunzi na hawakuona kosa lolote kwake ndiyo maana hawakumkamata, sasa iweje mkuu wa mkoa aje na amri.
 
Akizungumzia nguvu iliyotumika katika kumkamata Lema, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) Mkoa wa Tanga, Aaron Mashuve, aliliomba Jeshi la Polisi kuelekeza nguvu kama hizo katika kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).
 
Alisema nguvu hiyo kama ingetumika wauaji hao wangekuwa wamekamatwa badala ya polisi kupoteza muda kuhangaika na wanasiasa ambao wanaweza hata kuitwa kituoni wakaenda kwa hiari yao.
 
Katika hatua nyingine, CHADEMA mkoani Arusha kimetangaza kumfungulia mashtaka mkuu wa mkoa huo kwa tuhuma za kumtishia mbunge wao kwa ujumbe wa maandishi, pia kumtaka athibitishe madai ya kuwa kifo cha mwanafunzi kina uhusiano na masuala ya kisiasa.
 
Katibu wa mkoa wa chama hicho, Amani Golugwa, alisema taratibu za kuyashughulikia masuala hayo yote mawili zinaendelea chini ya jopo la wanasheria wa chama hicho

habari zenu

habari zenu wakazi wa mji wa himo