Friday, May 10, 2013

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU WAPEWA KICHAPO KIKALI BAADA YA KUNASWA WAKIJIUZA





WAREMBO watatu wanaodaiwa kuwa ni madenti wa chuo kikuu kimoja jijini Dar, waliojitambulisha kwa jina mojamoja, Rachel, Neema na Suzan, wamekumbana na balaa zito baada ya kupokea kibano cha kutosha...

Tukio hilo lilitokea maeneo ya Kijitonyama, jijini Dar, usiku wa saa 8:00, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo madenti hao walipokea kichapo  kikali  kutoka kwa Polisi Jamii.

Warembo hao walifikwa na kasheshe hilo baada ya kugeuka kero kwenye geti la kigogo mmoja  kwa kuwa walionywa mara kadhaa kuacha kupanga foleni katika eneo hilo na kujihusisha na vitendo vya ngono.


“Unajua walikuwa kero sana. Yaani asubuhi kukicha utakuta mipira ya kiume imetapakaa kila sehemu. Mbaya zaidi utakuta watoto wakicheza mchana wanaokota hiyo mipira ya kiume na kupuliza kama puto,” alisema shuhuda mmoja aliyeamshwa na makelele ya warembo hao wakati wakila kibano.
Aliendelea: “Unajua wakikaa hapa ni hatari tupu kwani wanaume wanaokuja kuwafuata wanaweza wakatudhuru kwa sababu hatuwajui.”


Katika tukio hilo, walinzi hao wakiwa kwenye doria, walipokea malalamiko kwa mara 1000, kutoka kwa kigogo huyo akiomba msaada wa kuwaondoa warembo hao getini kwake wanaodaiwa kujiuza eneo hilo.

Habari nyingine zilieleza kuwa wadada hao wamekuwa wakiweka mitego yao nje ya nyumba hiyo ikidaiwa kwamba lengo ni kumnasa kigogo huyo ili kumuuzia biashara yao kwa kuwa ni ‘mkataji’ mzuri wa mkwanja.

Mbali na hilo, pia ilidaiwa kuwa wanaume wapenda ngono rejareja na hatarishi huwafuata eneo hilo kupata huduma yao.
Ilidaiwa kuwa walinzi hao walielezwa kuwa katika kukuza biashara hiyo haramu, warembo hao wamekuwa wakiwabugudhi wakazi wa eneo hilo hadi kufikia hatua ya kuwagongea madirishani na kusimamisha magari hovyo

Huku wakijua wamepata wateja, kundi la kinadada hao wakiwa na vinguo vya kimitego na wengine kujifunua na kubaki nusu utupu ili kuwaonesha wanausalama hao nyeti zao wakijua ni wateja ndipo wakakutwa na kasheshe hilo.



Wanausalama hao, bila kuchelewa waliwazingira warembo hao na kuwanasa kisha kuwapa kibano lakini katika purukushani hiyo wengine walifanikiwa kupata upenyo na kuchoropoka.

Katika kibano hicho, makelele ya warembo hao yalisababisha watu kuamka na kufunga mtaa.
Kutokana na timbwili hilo la akina dada hao kuwa zito, iliwabidi polisi hao jamii watumie nguvu ya ziada kuwatuliza kabla ya kuwapeleka mbele ya sheria.

Baada ya warembo hao kudakwa, walipakizwa kwenye Bajaj na kupelekwa kituo cha polisi ili wafikishwe mahakamani.

No comments:

Post a Comment