Monday, May 13, 2013

SAFARI YA WANAJESHI WETU HUKO KONGO NA MBINU ZA KITOTO ZA WAASI WA M23

Watanzania  tunafuraha kubwa  kwa  sababu wapiganaji wa Jeshi letu  la Wananchi Tanzania (JWTZ) wamewasili mji wa Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kujiunga na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani  wakiwa  salama....


Wiki iliyopita, Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete alikabidhi Bendera kwa Kiongozi wa Bataliani ya wapiganaji wa JWTZ wanaokwenda nchini humo, kwenye hafla iliyofanyika Msangani Kibaha, Mkoa wa Pwani.....

Siku moja kabla ya kufika kwa kikosi cha pili cha Tanzania (cha kwanza kilienda kimya kimya) waasi wa M23 waliendesha kampeni kubwa sana ya kuhamasisha wananchi wa GOMA waandamane kupinga ujio wa askari wa Tanzania mjini GOMA...

Kiongozi wa siasa wa M23 akiongea na wakazi wa Kibumba na huku hutuba yake ikirushwa na redio inayomilikiwa na waasi na kusikika mjini GOMA ,aliwaasa wakazi wa GOMA wafanye maandamano makubwa siku vikosi vya TANZANIA vitakapowasili...

CHAKUCHEKESHA  ni kwamba, tofauti na waaasi walivyo tegemea , hakuna Mtu hata mmoja aliye andamana! Hii inaonyesha wazi  kuwa waasi hawa wameshapoteza ushawishi walio kuwa nao hapo awali....


PROPAGANDA ZA  UONGO WA M23
Waasi wa M23 wamekuwa wakiendesha vita ya kisaikolojia ya kuvichonganisha vikosi vya UN na wakazi wa jimbo la Kivu wenye asili ya kitusi....

M23 wamekuwa wakifanya mikutano ya hadhara na kusambaza vipeperushi kuwa WATANZANIA wamekuja kumsaidia KABILA kuwateketeza WATUSI (maauaji ya halaiki) kitu ambacho si kweli....

TUJIULIZE..!!! ..Kuna watusi wangapi wanaoishi Tanzania? si tungeanza na hao kama ndio lengo letu! ...Hayo  ni  maneno  ya  mfa  maji..!!!
  
Timu ya utangulizi ya ICGLR ambayo  ripoti yake ndo ilitumika na AU na baadaye baraza la usalama la umoja wa mataifa kupitisha azimio la kupeleka BRIGEDI yakuingilia kati  mzozo wa Kongo ilikuwa na makamanda kutoka majeshi yote ya nchi za maziwa makuu zikiwemo nchi za Rwanda, Uganda, Congo, Burundi nk: 

Makamanda  hao  walienda mjini Goma mwezi wa tisa mwaka jana wakiongozwa  na Brigedia jenerali James Mwakibolwa .Sasa kama lengo letu ni kuteketeza watusi , je, Rwanda ingekubali kweli?....Hayo  ni  maneno  ya  mfa  maji..!!!

Hata mazoezi ya awali ya kupambana na vikundi hatarishi kwenye nchi za ukanda wa Africa mashariki yalifanyika RWANDA  chini  ya  jina  la The Command Post Exercise (CPX)....

Mazoezi hayo   yaliongozwa na Brigedia jenerali James Mwakibolwa akisaidiana na Brig. Gen Jacques Musemakweri wa Rwanda. Hili la kuangamiza watusi ni kuweweseka kwa M23....


TUMESHAVUA  NGUO, NI LAZIMA  TUOGE..!!
Watanzania wengi ni watu wa kulaumu, wengi wanasubiri baya litokee kwa askari wetu huko DRC basi waanze kulaumu...

Ni  Vyema  serikali ikaanza kutuandaa watanzania  kwa
 kuendesha semina kwa waandishi wa habari  kuhusu  uzalendo  wa  nchi  yetu...

Mfano mzuri ni MALAWI, wao kwa sasa kwenye mzozo wa ziwa nyasa waandishi wote na taifa kwa ujumla bila kuzingatia vyama vyao wala dini wako kwenye "state of union" ...


Nachukulia  mfano  mwandishi wa makala wa gazeti la nyasa times ( Malawi Nyasa Times - Malawi breaking news in Malawi ), Patricia Masingaambaye  kwenye makala yake ya tarehe 5 mwezi huu amewafananisha viongozi wa Tanzania na Adolf hitler! ....


Patricia  anadai  Tanzania ni wapenda vita  na ndo maana tunag'ng'ania ziwa malawai (ziwa nyasa) ...Mwandishi  huyo  ameandika kuwa tunag'ang'ania kwenda CONGO kwa ajili ya mali iliyoko CONGO na tunang'ng'ania ziwa malawi kwa kuwa chini yake yamegundulika mafuta na gesi! ...


Patricia Masinga pia anadai watanzania hatujui kiingereza ndio maana tumeng'ng'ania tunaushahidi wa uongo...


Naye mhariri wa NYASA TIMES katika kile alicho kiita TAHARIRI MAALUM ya tarehe 28/2/2013 alidai kuwa kama TANZANIA tunataka nusu ya ziwa nyasa basi turudi kwenye win - win situation,  yaani turudishe ardhi yote iliyokuwa chini ya utawala wa MARAVI KINGDOM ambayo ilitawala eneo kubwa la kusini mwa Tanzania kabla ya kuja wakoloni .

Haya ni  matusi makubwa kwetu  na  juhudi  za  wenzetu  kuzitetea nchi  zao .Nadhani hii ni chachu  tosha  kwa  waandishi wa habari wa  Tanzania  ....

Tuuvue  UCHAMA  na  badala  yake  tuuvae  UZALENDO  ili Tuilinde Tanzania ya Kesho..!!

No comments:

Post a Comment