Wednesday, May 8, 2013

MWENYEKITI WA BARAZA LA MITIHANI - (NECTA ) ANADAI KUWA HAYUKO TAYARI KUYABADILI MATOKEO YA KIDATO CHA NNE -2012


Kuna  tetesi  kwamba  Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu Mkuuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwekaza Sympho Mukandala amegomai kubadili matokeo ya Kidato cha Nne- 2012.

Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa.

 "Sisi tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa elimu ya wapi?" alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala.

Habari za kuaminka zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo. 

Hata  hivyo, siku  za  hivi  karibuni  mwanahabari  wetu  alizungumza  na  Ofisa Habari wa NECTA, John Nchimbi ambaye alisema wamekwishapokea maelekezo kwa barua na kufanyia kazi ili kujitahidi ndani ya muda mfupi matokeo yawe yametoka.

Nchimbi alikiri kuwapo kwa kasoro katika matumizi ya mfumo huo mpya wa usahihishaji, kwani hawakushirikisha wadau wengi kabla ya kuanza kutumia, lakini lengo la Baraza lilikuwa jema katika kukuza elimu nchini
“Kutokana na tangazo hili, wanafunzi hawa wote hawana matokeo tangu juzi ( yalipofutwa bungeni ), hivyo wasubiri matokeo mapya yatakayotangazwa, na waelewe wazi kuwa si lazima waliofeli wafaulu wote,” alisema  Nchimbi.

--->Ngoja  tuone  hatima  ya  vita  hii  ya  WANASIASA  na  WANATAALUMA 

No comments:

Post a Comment