Mbunge Msigwa amesema kuwa katika
ukweli hatakuwa tayari kumwogopa mtu na kuwa siku zote atasimama
katika ukweli katika kupigania maslahi ya Taifa hili.
Mbunge Msigwa amesema kuwa hatua ya
katibu mkuu wa CCM kukimbilia katika vyombo vya habari kutishia
kumfikisha mahakamani bila yeye mhusika kupelekewa taarifa ni sawa na
kumwogopa na hivyo suala la Kinana kwenda Mahakamani si sawa ni
kumtishia nyau mtu mzima.
Msigwa alisema Chadema ina mawakili waliojitosheleza na kuwa hawatanyamaza kusema ukweli kwa kuogopa vitisho vyovyote .
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini
akiwahutubia umati mkubwa wa wananchi wa jimbo hilo leo jioni katika
eneo la stendi kuu ya mabasi ya mikoani
Umati mkubwa wa wananchi wakimsikiliza mbunge wao wa jimbo la Iringa mjini
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji ,Msigwa akiwahutubia wananchi wa jimbo la Iringa mjini
No comments:
Post a Comment