Thursday, May 16, 2013

MAHAKAMA YA IRINGA YAKANUSHA POLISI KUMSHIKILIA MLINZI WAKE KWA KUIBA BANGI



MAHAKAMA kuu ya Tanzania kanda ya Iringa  imepinga  vikali taarifa ya  jeshi la polisi mkoa  wa Iringa (RPC) Michael Kamuhanda  aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari  kuwa inamshikilia mtumishi  wa mahakama hiyo kwa kuiba bangi iliyofikishwa mahakamani hapo kama kielelezo.

"Taarifa ya kamanda wa polisi kuwa bangi imeibiwa mahakamani si ya kweli na imelenga kuichafua mahakama. Mahakama hawajapata kuibiwa. Taarifa hizo si za kweli kabisa".

Akizungumza na  wanahabari  leo ofisini kwake kaimu msajili  wa  mahakama kuu Tanzania kanda ya Iringa Godfrey Isaya alisema mahakama inasikitishwa taarifa ya Jeshi la polisi inayoupotosha umma kwa kutoa taarifa ya 

uongo bila kufanya uchunguzi.

Amesema kungekuwamo kuibwa vielelezo, ilipaswa kuwepo kwa mlalamikaji ambaye ni Mahakama kwenda kufungua kesi polisi.

 Tunakanusha  vikali kuwepo kwa  upotevu  wa kielelezo cha bangi katika mahakama hii Exhitibit Room haijavunjwa iko intact... tulikuwa na kielelezo P.3 katika shauri  hilo la jinai namba 24/2012 ambayo ni bangi  viroba 8 amri ya mahakama ya kuteketeza ilitolewa tarehe 13/2/2013 na bangi  hiyo iliteketezwa chini ya uangalizi  wa afisa wa  jeshi la polisi na kesi hiyo  ilikwisha tarehe 13 /2/2013 na mshtakiwa alihukumiwa kifungo cha miaka miwili  jela."

Alisema kama ilivyokuwa katika kesi nyingine za jinai, “tunatoa wito kwa jeshi la polisi  Iringa kufanya uchunguzi wa kina kuona bangi hiyo imepatikana wapi kwa kuwa sisi hatuhusiki.”

Pia alisema kama kweli mahakama kuna vielelezo vilivyoibwa, basi polisi wangefika kufanya upelelezi hata  kuwahoji kama njia ya kuchunguzi .

"Tunalishauri jeshi la polisi kufanya utafiti wa kina kuhusu suala hili kabla ya kutoa taarifa katika vyombo vya habari"


No comments:

Post a Comment