Sunday, May 12, 2013

" HAKUNA KANISA LILILOSHAMBULIWA KWA BOMU JIJINI DAR LEO "...HII NI KAULI YA KAMANDA KOVA


Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kova amesema Taarifa zilizoenea kwamba Bomu limelipuka katika Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania (KKKT), Kunduchi jijini Dar es Salaam zimeenea ndivyo sivyo na kwamba askari walikuwa wanapambana na majambazi.

Wakati taarifa zikiwa zimesambaa katika mitandao ya kijamii na mitaani kwamba kuna kanisa la KKKT limeshambuliwa na bomu hivi punde, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kova amesema kwamba taarifa hizo sio za kweli na kwamba askari wa jeshi la polisi walikuwa wanapambana na majambazi karibu na eneo la kanisa hilo. 


Katika mapambano hayo polisi waliwarushia majambazi hayo bomu ili kuyakamata.

"Wakati askari wetu wanapambana na majambazi hayo- waumini wa kanisa hilo wamejitokeza kuwasaidia askari wetu. Naomba unisaidie kukanusha siyo kweli, nitazungumza na vyombo vingine vya habari kuweka sawa," amesema Kamanda Kova hivi Punde.

No comments:

Post a Comment